MSINGI WA KARATASI YA PILI (102/2) ~ ni kitabu kilichoandaliwa kwa ustadi sana. Kitabu hiki kinalenga kuwasaidia watahiniwa wa shule ya upili katika kuelewa mabadiliko ya kimtindo ya utahini wa karatasi za Kiswahili kutoka kwa kanseli ya KNEC.
Mitihani ya kitaifa ya siku hizi imebadilika na maswali yanahitaji watahiniwa kuwaza kwa kina basi ni vyema kutambua vipengele hivyo muhimu vinavyotahiniwa sasa, kuvichambua na kuviweka wazi ili mambo yasiwe mrama.
Kitabu hiki kimezingatia mambo yafuatayo:
- Maelezo kuhusu namna ya kushughulikia vifungu vya ufahamu. Maelezo haya yatamfaa mwanafunzi kumudu alama nzuri katika sehemu ya ufahamu.
- Ufafanuzi kwa kina kifaacho kuhusu vifungu vya Muhtasari utakaomwezesha mwanafunzi kumudu maswali ya ufupisho.
- Uwasilishaji murua na unaoleweka kwa vipengele tofauti tofauti katika sarufi na matumizi ya lugha
- Maelezo mazuri katika kitengo cha isimujamii. Maelezo haya yatampa mwanafunzi mafunzo kuhusu namna ya kutumia lugha katika miktadha tofauti tofauti.
Reviews
There are no reviews yet.