Baada ya kuzindua Uhakiki wa Fasihi na Isimujamii, kulikuwa na haja ya kuzindua Uhakiki wa Sarufi na Insha. Sarufi ni mojawapo wa mada muhimu katika karatasi ya pili ambayo inazidi kuwatatiza wanafunzi wengi. Vitabu vingi vya sarufi vimeandikwa lakini kuna haja ya kuingiza masuala ibuka katika sarufi. Kitabu hiki kimeweza kuangazia masuala ibuka katika utahini wa sarufi. Vipengele kama vile kiima, kiarifu, chagizo, kijalizo, uchanganuzi wa sentensi kwa njia ya mistari na mstari, kirai, kishazi ni vipengele vingine vimeangaziwa kwa kina katika kitabu hiki.
Reviews
There are no reviews yet.