Kwa kweli nilighairi kwamba ujana,si ujana tu ila usipochunga utapata vidonda na makovu yatakayo kukumbusha mengi.Ua la waridi umetameta na kunukia siku ya kwanza lakini baada ya muda unyauka na kupoteza umbo lake la kupendeza. Wazo hili lilinijia nilipokua nikijinasua katika mawazo yangu baada ya tukio ambalo liliwaacha waja wa Adamu na Hawa vinywa wazi katika Chuo Kikuu Cha Ubora Kusini mwa bonde la ufa, nilikua mwanafunzi wa mwaka wa tatu nikifanya taaluma ya utangazaji na mawasiliano. Machweo siku ya ijumaa, kila mtu akiwa katika shuguli zake kuelekea darasani kupata maarifa,nikiwa katika mwendo wa kasi nilipatana na shogangu Pamela ingawa...
JINAMIZI LA UJANA
