Blog

Barua Kwa Moyo na hadithi nyingine

Dunia inapita kwa Kasi sana. Wakati nao hausimami. Jua nalo lakimbia. Ni hali hizi na nyingine ambazo  zimemfanya binadamu kujipata katika tanzu zinazotatiza na changamoto changamano chungu nzima. Maradhi, siasa duni, ufisadi, dhiki, ushirikina, mateso, chuki, mauti, vita, elimu, uongozi mbaya, utamaduni, kisasi, wivu, ubaguzi, ugatuzi, afya, ulevi, shinikizo, bidii, ari, hiari, uvumilivu, subira, ufanisi, ushindi  na mapenzi ni baadhi tu ya mambo yanayomkabili mlimwengu katika dunia yake. Fasihi ndicho kioo au video aula ya kuyaweka

makabiliano ya mja na ulimwengu hadharani. BARUA KWA MOYO WANGU na HADITHI NYINGINE ni fasihi iliyosukwa kwa ustadi ili kuyaweka wazi mapito ya mja tangu utotoni hadi ukubwani. Ni diwani ya kusomwa na mtoto ili aelewe maisha ya wazazi na mzazi aelewa

maisha ya mtoto. Kiongozi akiisoma ataelewa mahitaji ya raia na raia atajua majukumu ya kiongozi.

Hadithi zimesukwa kwa msuko na mnato. Misamiati,tamathali,fani na mbinu za Lugha zimetumika kumpa msomaji dira ya kumwongoza

kuifahamu jamii yake vizuri. Waandishi ni walimu na watahini wa

mitihani tajika nchini. Tajriba yao imejiweka wazi katika hadithi zao za kusoma na kusoma tena.

Wahariri: Kaka Fred na John ‘Ustadh’ Kamau ni walimu wenye tajriba ya kusemwa na kutambulika. Wameshiriki katika vipindi na makongamano mengi ya makuzi ya Lugha. Aisee! Asomaye Antholojia hii

anajisoma yeye na jamii yake. Usikose.

Barua kwa Moyo Wangu na Hadithi Nyingine-client order

Leave your vote

More

Leave a Comment

Your email address will not be published.

You may use these HTML tags and attributes:

<a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

Add to Collection

No Collections

Here you'll find all collections you've created before.

Open chat
1
Elong'o Publishers Support Team
Hello 👋
How can we help you?
Call Now Button