Bi. Jane Mumia ni mwalimu mwenye tajriba ya miaka mingi katika ufundishaji wa somo la Kiswahili. Alisomea katika shule ya msingi ya  Mtakatifu Charles Lwanga Koromaiti kule

Chekalini. Kwa miaka sita aliendeleza masomo yake ya 

sekondari katika shule ya wasichana ya Butere (BGHS) na kumilikishwa vyeti vya EACE na KACE mtawalia. Hatimaye, Bi. Mumia alisomea shahada ya ualimu katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta kisha shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu Cha Moi. Bi. Mumia amefundisha Kiswahili katika shule nyingi hapa

nchini. Amefundisha katika shule ya upili  ya wasichana ya Kapsabet, St. Augustine-Lukhuna Girls, Bishop Philip Anyolo Boys High School-Kakamwe, Namunyiri Girls na Michael Wamalwa-Kakimanyi. Hivi sasa, Bi. Mumia amestaafu akiwa mwalimu msimamizi katika shule ya upili ya Mtakatifu. Maria Magdalena-Siloba. Anatizamia kuanza shahada yake ya uzamivu muda si mrefu.