Msheshe. R. Rashid, ni mwalimu mkomavu, mshairi wa enzi mpya maarufu Kwa lakabu ya Msese wa Kondeni. Ni miongoni mwa waandishi chipukizi aliyeshiba uzoefu na umilisi wa lugha ya kiswahili. Ana tajriba Pana katika kuchangia ujenzi wa maendeleo ya kiswahili. Msururu wa mkono wake wa uandishi upo kwenye Hadithi nyingine kama:Kipepeo mdogo,Kijijini Shebele,Vifaranga wenye Rangi, Barua kutoka Ng’ambo na Diwani ya Mwana Msikivu miongoni mwa vitabu vingine vingi.