Ndeda Vitalis Nadecho ni mwalimu mwenye tajiriba na vilevile mwandishi wa kazi za Kiswahili. Ameandika kazi kadhaa zikiwemo Diwani Ya Mwamba Wa Dhahabu na Hadithi Nyingine, Diwani ya Wosia na Mashairi Mengine na nyingine nyingi. Anapania kukuza viwango vya usomaji wa Kiswahili kwa wanafunzi wa viwango vyote.