Blog

JINAMIZI LA UJANA

Kwa kweli nilighairi kwamba ujana,si ujana tu ila usipochunga utapata vidonda na makovu yatakayo kukumbusha mengi.Ua la waridi  umetameta na kunukia siku ya kwanza lakini baada ya muda unyauka na kupoteza umbo lake la kupendeza.

Wazo hili lilinijia nilipokua nikijinasua katika mawazo yangu baada ya tukio ambalo liliwaacha waja wa Adamu na  Hawa vinywa wazi katika Chuo Kikuu Cha Ubora Kusini mwa bonde la ufa, nilikua mwanafunzi wa mwaka wa tatu nikifanya taaluma ya utangazaji na mawasiliano.

Machweo siku ya ijumaa, kila mtu akiwa katika shuguli zake kuelekea darasani kupata maarifa,nikiwa katika mwendo wa kasi nilipatana na shogangu Pamela ingawa kwa sasa hakuwa mwandani wangu kabisa, bado nilimwona kama rafiki wangu wa dhati sana.Tuliamukuana:

“Pamela mambo”,nilimuamkua.

“Poa sana” alinijibu kwa sauti nyonge.

“Mbona unaonekana kuboeka hivyo?au bado mwili wako wakutatiza?nikamuuliza.

“Ngrrrh!hata usiniulize utanifanya nipoteze moods zangu manze”,  alinijibu.

m.m.m.m.h sawa nilimjibu nikisitasita huku maswali kadhaa yakinipita akilini mwangu.Sikuwa na budi ila nilisalimu amri ya kuendelea kumuuliza maswali hayo ,hata hivyo nilikuwa na hamu na ghamu  kujua yaliyomfika  kidosho huyu wa umri wangu kusongwa na mawazo namna hiyo.

* *  *

Naam Pamela alikuwa ni kitinda mimba katika familia ya wana saba,alijaliwa kulelewa na wazazi wote wawili.Babake alikuwa mwalimu mstaafu wa shule ya msingi kadhaa katika eneo hilo la Setini  upande wa Bonde la Ufa ambamo tulikua katika eneo moja la ugatuzi  lakini maeneo tofauti.Mwalimu huyo alionekana kama shujaa kwani alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupata na kufaidi elimu ya mabeberu wakati wa ukoloni nchini.Fauka ya hayo alikua mtu mcha mungu sana,alikua miongoni mwa viongozi wa kanisa katika maeneo hayo.

Kutokana na kulelewa katika familia wacha mungu,Pamela alikuwa ni  msichana mpole na mtiifu,mwenye siha nzuri  na adhabu iliyoonewa gere na akina mama wa kijiji kwani mabinti zao walikua kinyume na tabia za Pamela kwani walizurura na vijana na hata kuvaa mavazi yasiyopendeza mbele za wazazi wao.Alikuwa wa kupigiwa mfano.

Aidha Pamela alikua wembe shuleni kwani kazaliwa na maarifa na hata uwezo wa kuelewa mambo haraka sana si hesabati,si biolojia,si somo la dini,si kemia yote alikua akielewa kwa ufasaha mwingi sana.Wengine wetu hesabati ilikua changamoto kubwa kwani tulienzi lugha sana hasa Kiswahili na somo la kiingereza.Aliweza kufuzu vyema katika mtihani wake wa kidato cha nne na alama ya A(-) na kuweza kuitwa katika chuo hiki moja ya Ubora ambapo alitakikana kusomea taaluma ya uandisi.Taaluma hiyo ndiyo bora na gumu zaidi katika chuo hicho na hasa ni nadra sana kupata mabinti wakiisomea kwani imeamiika ni ya wanaume pekee!

*

Nakumbuka vyema tulipatana na Pamela katika foleni tulipokuwa tukisajiliwa siku ya kwanza Chuoni .Msichana rangi ya maji ya kunde,mwili wa kati,kava sketi lililomsetiri vizuri hadi miguuni,fulana nyeupe na kafunga kichwa na kitambaa nyeupe-kwani kanisa aliyosali mabinti na  akina mama hawakuruhusiwa kufungua vichwa zao, eti ni dhambi!sijui lakini sikutaka kuuliza zaidi…

Katika harakati za kusukumana na kungangana foleni,kila mtu kachoka baada ya safari ndefu,mamake Pamela aliweza kuja kumnongonezea jambo ,nilipogundua kuwa alitoka katika jamii moja na lile langu.

Nilishusha pumzi kwa kuwa nilkuwa nimehisi kwamba nilkuwa pekee,kwani wengi tuliokuwa foleni wote walionekana na kusikika kama wana wa miji mikuu kama vile Nairobi na Mombasa.Walioongea lugha hasa ya kiingereza kwa ufasaha mwingi kinyume na mimi niliyekuwa na uwezo tu ya kuandika lakini kwa ndimi ilikuwa kikwazo!

Baada ya kusajiliwa kila mmoja aliweza kuelekea katika vyumba vyao mapya kwani vyumba vya shule zilikuwa chache mno na tulipofika wengi walishanyakua nafasi hizo.

Leave your vote

This post was created with our nice and easy submission form. Create your post!

More

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes:

<a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

Add to Collection

No Collections

Here you'll find all collections you've created before.