Elong'o Publishers

Bohari la Ushairi

500.00 /=600.00 /=

  • Author: Duke Nyakundi
  Ask a Question

Bohari la ushairi ni mojawapo ya diwani ya ushairi ambayo imesukwa na watunzi mashuhuri wenye tajriba komavu. Ni diwani yenye upekee wa aina yake ambayo imedadavua utanzu wa ushairi kwa kina ili kuwafaa wasomaji na hadhira lengwa. Istilahi muhimu za kishairi zimechambuliwa kwa upevu mno. Bahari zote za mashairi zimechambuliwa huku mifano anuwai ikiangaziwa.

Imejumuisha watunzi shupavu kutoka taifa la Kenya na Tanzania.

Waandalizi: Duke Nyakundi, Mildred Musimbi, Francisca Wambua, Robert Nyakundi na Meshack Wilson Mgoja ni magwiji waliobobea kwenye ushairi. Wamefanikisha tanzu nyinginezo za fasihi kama vile hadithi fupi, riwaya na tamthilia.

Diwani hii imehaririwa kwa ustadi na wahariri mahiri ambao pia ni vigogo wa fasihi na wataalamu wa lugha ashirafu ya Kiswahili. Wahariri ambao wamefanikisha miswada ya kila aina ikiwemo magazeti, hadithi fupi, tamthilia, riwaya na nyinginezo kwenye mashirika mengi ya uchapishaji. Macho hayafilisi kitabu. Nyanyuka ukakitafute ili umakinike mbeleni!

 

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Bohari la Ushairi”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

No more offers for this product!

General Inquiries

There are no inquiries yet.