“Nitazame vizuri, miimi mimi Salima Habibu, waridi la utamu wake, moto wa kuotea mbali. Salima kipenzi cha watu, tubishane nini na kibaraka wewe…” Inakuwaje hata Salima Habibu – bikira mtarajiwa, aliyelelewa kwa itikadi kali za kidini – kubadilika kiasi cha kufuru? Ni kweli ni bikira, ni nini hasa kilichomfanya awe bikira na, atakwepaje visiki katika aushi yake ambayo inaingia usaha? Ni kwa nini aisaliti dini? Kwa nini amsaliti Sista Joyce aliyejikusuru kama chungu ajengaye kichunguu kumlea katika mwanga?
Kivuli cha Usaliti ni riwaya inayomsisimua msomaji katika masimulizi yaliyotiwa nakshi, yenye kusisimua na kumleta msomaji katika ulimwengu halisia. Ni riwaya ambayo inaangazia usaliti, mapenzi, chuki, kisasi, anasa na uozo katika jamii ya kisasa na kuibua dhana mbalimbali ambazo msomaji anapaswa kutafakari.
Reviews
There are no reviews yet.