Kishindo chochote cha sauti kinaposikika, mtu hupatwa na hisia zitokanazo na wito wa ujumbe katika sauti hino. Sauti zaweza kuwa za vicheko wakati wa furaha, vilio wakati wa majonzi, lalama wakati wa dhuluma, nasaha au wakati ambapo maovu yameshitadi. Baadhi ya sauti ni za kimya kimya wala hazisikiki kwa masikio bali watu huhisi kemi na mwangwi wake moyoni. Sauti hizi zimo akilini mwa waja ambao wanapitia mapito anuwai ya dunia.
Washairi wameteremshiwa uwezo wa kupaza sauti hizi. Na kama ilivyotajwa hapo mbeleni, sauti za washairi zinasikika kutokana na kalamu zao. Kila kalamu zinapomwaga wino, tunapata kufunguliwa kurasa za maisha ya kawaida ya waandishi hawa; maisha ya jamii zao, utamaduni wao, mapito yao, dhiki zao, faraja zao na ndoto zao. Hawaandiki kwa huzuni kwa kutaka kwao bali hayo ndiyo wanayopitia. Na hivyo ndivyo wanavyofanya wanapoandika kwa ajili ya kunasihi na kupumbaza. Diwani imehaririwa na kuhakikiwa na waandishi wenye tajiriba kubwa kwenye tasnia ya uandishi wa hadithi na utunzi wa mashairi. Sikiliza sauti zao kwa makini!
Reviews
There are no reviews yet.