Elong'o Publishers

Ulichipuza Ukatani

150.00 /=500.00 /=

  • Author: Maelo W. Morgan
  • Edition: 1st
  • Language: Swahili
  • Publisher: Elong'o Publisher
  Ask a Question

Ulichipuza Ukatani

“Niliwanyamazisha.” Mleka alijibu. “Usiniambie umeuwa!” Mumini alishangaa. “Ni kazi yangu kuwakomesha wahalifu.” Mleka alisema huku akiangaza macho chumba hicho. “Chumba hiki ulikipaka rangi tofauti. Si mbaya.” Mleka alitamka. Katika hiyo harakati ya kukikagua chumba hicho aliiona ile simu ya kijipembe ambayo Mumini alikuwa ameitupa kitandani. Aliitazama kwa muda kisha akaichukua akaanza kuikagua kwa makini. Alionekana kushtuka baada ya kuikagua simu ile. “Hii simu ni ya nani?” Mleka aliuliza. Mumini alikuwa amesahau kuwa alikuwa ameitupa simu hiyo kitandani. Alishtuka kuulizwa swali hilo. “Haijalishi. Umekuja kuungalia vitu vyangu ili kuniuliza maswali ya kipumbavu au umekuja kwa kuogopa upweke?” Mumini aliuliza.

 

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Ulichipuza Ukatani”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

No more offers for this product!

General Inquiries

There are no inquiries yet.