UJASIRI

Author(s): Mayfair Wanja

About this book

UJASIRI  ni hadithi kuhusu changamoto anazopitia mtoto wa kiume. Ni  hadithi ambayo imemchora mtoto wa kiume kama mtu jasiri ambaye  anaweza kufaulu licha ya kukumbwa na changamoto  nyingi  katika maisha.

Inamhimiza mtoto wa kiume kutokata tamaa, kuwa na  matumaini na pia kuwa na ruwaza ya kufanikiwa maishani.   Mwanamume / mtoto wa kiume anahitaji kutiwa moyo, kushikwa mkono katika safari ya maisha na ataweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii, kama vile tunavyomwona mhusika mkuu Bwana Suluhu akikumbwa na masaibu mengi kama vile: kuchomewa nyumba, kufukuzwa nyumbani, uchochole uliokithiri ,bibi yake kutoroka na kumwachia jukumu la kuwalea wanao peke yake, kuugua saratani na kuweza kuishinda na kupona, kuachwa na bibi wa pili na masaibu mengine mengi  lakini licha ya haya yote alijikaza kisabuni  na akaweza kufanikiwa mwishoni.  Kupitia hadithi hii tunaona kwamba kila kitu kinawezekana sio tu kwa wanaume   bali kwa yeyote  aliye na  ujasiri na msukumo wa kufaulu maishani. Tunahimizwa tusife moyo kwani tukijitahidi tutaweza kushinda changamoto zote.