Ndipo maendeleo yapatikane, lazima wanajamii wachague viongozi wenye maono, mbinu na bidii ya kufanikisha maendeleo. Kiongozi anayefahamu mahitaji ya wananchi na kujitolea kwa hali na mali kuyashughulikia ipasavyo ndiye anayestahiki kupewa fursa ya kuongoza. Kumbuka, uongozi bora, maisha bora.
Nyota ya Maendeleo ni kitabu kinachochora picha kamili kwa namna Mheshimiwa Dr. Didmus Barasa alivyo kiongozi mwenye rekodi bora ya maono, mbinu, moyo, bidii na uwezo wa kufanikisha maendeleo.