BOOK category

Hangaiko

About this book

Subira, mwanamke mrembo kweli anabahatika kuolewa na tajiri aliyesifika sana aliyeitwa Bw. Hamisi aliyekuwa na sifa maridhawa. Ingawa hivyo, ndoa ya Subira ina doa. Anajikuta katika bahari kubwa ya fadhaiko lisiloliwazika. Mume wake naye ameathiriwa na swala la tathmini na falsafa ya maisha, huishi kutafuta chanzo na suluhu ya kuhangaika kwa binadamu.

Stela, kijakazi wa Subira anajipata katika hali tamaushi ya maisha anapokosa pesa za kulipia karo ya kuingia shule ya upili. Fauka ya hayo, yeye anasadiki kuwa maisha yake siku moja yatang’aa kwa ufanisi.

Subira anajaribu kwa kila njia na jiha kupigana na teseko la ndoa yake asiweze na akawa anauona ulimwengu kama bahari tesi. Sasa swala likawa je, hatima ya Subira itakuwaje? Stela naye, atafikiwa na siku za ufanisi? Je, Bw. Hamisi atadakua siri ya uumbuji wa misuko na sakata ya maisha? Nayo hakika ikabaki kuwa hangaiko bila shaka ni kutaka ukakosa au pengine, kutafuta usipate!