MAISHA YANGU KITABU CHA KWANZA (1982 – 2020)
Maisha Yangu ni simulizi ya kweli ya safari ya maisha ya Ali Alio Abdullah; safari iliyojaa changamoto, matumaini, mapambano, mafanikio, makosa, majuto, na hatimaye faraja. Ni hadithi ya mtu wa kawaida aliyepitia nyakati ngumu, akiinuka mara kwa mara, akijifunza na kupata hekima katika kila hatua ya maisha.
Katika kitabu hiki, utasoma kuhusu utotoni, malezi, ndoa, shule, maisha ya kazi, safari za maisha, misukosuko mbalimbali, hadi ilivyomfikisha korokoroni, na vile alivyopata nguvu ya kusimama tena. Ni kumbukumbu iliyoandikwa kwa lengo la kuwaelimisha, kuwaongoza na kuwatia moyo vijana, wazazi, familia na jamii kwa ujumla.
“Mwelekeo wako ndio muhimu zaidi kuliko haraka yako.” — Ali Alio Abdullah “Kila maisha yana hadithi. Yangu hapa, kwa vizazi vijavyo.”