Sarufi: Kitabu cha Kuelewa sio cha Kukariri
Kiswahili Sarufi Gredi 6: Kitabu cha Kuelewa sio cha Kukariri kimeandaliwa maalum kwa wanafunzi wa gredi ya 6 ili kuwasaidia kuelewa kwa kina misingi ya sarufi bila kubahatisha wala kukariri. Kitabu hiki kinazingatia silabasi yote ya sarufi ya gredi ya 6 kwa lugha rahisi, mifano elekezi na mazoezi bora yanayojenga uelewa na kuongeza ufaulu.
Kitabu hiki kimegawanywa katika:
- Masomo sita muhimu yanayojumuisha silabasi yote ya gredi ya 6.
- Ufafanuzi wa kina ukisaidiwa na mifano rahisi.
- Mazoezi baada ya kila somo ili kuimarisha uelewa na kujenga imani ya mwanafunzi.
Kitabu hiki ni rafiki wa kweli wa mwanafunzi anayehenga kufaulu na kuijua sarufi kwa ufasaha.