Anyolewaye kwa chupa hawezi kusahau. Hakuna tuzo ipatikanayo kwa maovu. Antholojia hii imesawiri maudhui yatakayokupa motisha ya aushi. Imeyazamia masuala haya na kuchora taswira halisi ya jamii ilivyokuwa, ilivyo na inavyopaswa kuwa katika siku za halafu. Kitovu cha Hadithi ni kundi lililozalisha waandishi wenye tajiriba katika tasnia ya fasihi. Baadhi yao ni washauri na watahini katika mitihani ya kitaifa.
Kaka Fred na Mwalimu Sammy ni wahariri wenye ufundi mkubwa. Wamehariri makala mengi na kushiriki kwenye vipindi mbalimbali vya makuzi ya Kiswahili. Diwani hii ni tuzo kwako ewe msomi! Hutakosa kunakili kipya baada ya kusoma. “Kusoma kuna maarifa nayo elimu ipate vitabuni” Tomkim Seneta Barasa.
Reviews
There are no reviews yet.