Elong'o Publishers

Publish
Online Library
Rent A Book

Barua kwa Moyo Wangu

200.00 /=600.00 /=

  • Author: Elong'o Publishers
  • Edition: 1st
  • Language: Swahili
  • Publisher: Elong'o Publisher
  Ask a Question

Description

Dunia inapita kwa Kasi sana. Wakati nao hausimami. Jua nalo lakimbia. Ni hali hizi na nyingine ambazo  zimemfanya binadamu kujipata katika tanzu zinazotatiza na changamoto changamano chungu nzima. Maradhi, siasa duni, ufisadi, dhiki, ushirikina, mateso, chuki, mauti, vita, elimu, uongozi mbaya, utamaduni, kisasi, wivu, ubaguzi, ugatuzi, afya, ulevi, shinikizo, bidii, ari, hiari, uvumilivu, subira, ufanisi, ushindi  na mapenzi ni baadhi tu ya mambo yanayomkabili mlimwengu katika dunia yake. Fasihi ndicho kioo au video aula ya kuyaweka makabiliano ya mja na ulimwengu hadharani. BARUA KWA MOYO WANGU na HADITHI NYINGINE ni fasihi iliyosukwa kwa ustadi ili kuyaweka wazi mapito ya mja tangu utotoni hadi ukubwani. Ni diwani ya kusomwa na mtoto ili aelewe maisha ya wazazi na mzazi aelewa maisha ya mtoto. Kiongozi akiisoma ataelewa mahitaji ya raia na raia atajua majukumu ya kiongozi.

Hadithi zimesukwa kwa msuko na mnato. Misamiati,tamathali,fani na mbinu za Lugha zimetumika kumpa msomaji dira ya kumwongoza kuifahamu jamii yake vizuri. Waandishi ni walimu na watahini wa mitihani tajika nchini. Tajriba yao imejiweka wazi katika hadithi zao za kusoma na kusoma tena.

Wahariri: Kaka Fred na John ‘Ustadh’ Kamau ni walimu wenye tajriba ya kusemwa na kutambulika. Wameshiriki katika vipindi na makongamano mengi ya makuzi ya Lugha. Aisee! Asomaye Antholojia hii anajisoma yeye na jamii yake. Usikose.

 

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Barua kwa Moyo Wangu”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

No more offers for this product!

General Inquiries

There are no inquiries yet.