“CHOZI LA DAMU” ni riwaya inayosimulia kwa ustadi, kina na uketo wa kipekee maudhui ibuka yakiwemo: uele wa korona, ushauri – nasaha, uchochote, mafuriko, ujirani, uozo wa ndoa, mizuka, malezi na msongo wa mawazo. Nadhari na taswira halisi imechorwa na Bi. Katembo anayegura kutoka eneo la Kapweta na kuhamia kwingineko kutokana na adha za mvua ya kifuku pamoja na Bi. Mwaipaja aliyefiwa na jamaa wake sita mintarafu ya ukongo hatari wa KORONA.
Kwa minajili ya kumtega na kumpiga msomaji bakunja, Riwaya ya “CHOZI LA DAMU” imesukwasukwa na kufumwa kwa tamathali sampuli na nui za uandishi.
Reviews
There are no reviews yet.