Elong'o Publishers

Publish
Online Library
Rent A Book

Kitumbua cha Mauti

150.00 /=600.00 /=

  • Author: Elong'o Publishers
  • Edition: 1st
  • Language: Swahili
  • Publisher: Elong'o Publisher
  Ask a Question

Katika pilkapilka za kulivuka daraja la ukata ili kuupakata ukwasi, wapo watumiao njia mkato na wapo wajitumao kwa bidii na haki wakimaizi kuwa hawafai kuwa kupe. Kitumbua cha mauti ni antholojia iliyosukwa ikasukika kama mswala.

Imejumuisha waandishi wenye utaalamu wa hali ya juu na wenye macho mapevu yaliyoangaza maudhui ya kisasa. Inajivunia anwani anuai zenye mafunzo ya hekima na tabasuri zinazotahadharisha na kueneza injili ya usawa na kupinga mitazamo hasi katika jamii ya wanaleo. Wahariri wamepiga mbizi na kuzuka na upanzi muafaka utakaokufanya ukienzi Kiswahili na fasihi. Kaka Fred, Ustadh Kamau na Okwalo Wambani ni mfano tosha wa wahariri mahiri wa fasihi.

Visa vina tamathali aali aali zitakazomfanya msomi kutoiweka chini nakala hii. Ama kweli hutahema na kushika tama kwa kujinyakulia diwani hii. Usingoje kuhadithiwa jamani! Kaa mkao wa kula ule shibe yako.

 

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kitumbua cha Mauti”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

No more offers for this product!

General Inquiries

There are no inquiries yet.