Elong'o Publishers

Publish
Online Library
Rent A Book

UCHUNGU WA MWANA na Hadithi Nyingine

  • Author: Elong'o Publishers
  • Edition: First
  • Language: Kiswahili
  • Publisher: Elong'o Publishers

This product is currently out of stock and unavailable.

  Ask a Question

Description

Baina ya siku ya kuzaliwa na ya mauti, binadamu hukumbana na kukabiliana na pandashuka kemkem. Bi. Safari anajua hili fika.

Maisha yake yamemwonjesha asali na shubiri  kwa wakati mmoja. Analazimishwa ndoa na baba yake aliyemkuza katika maisha ya fimbo mkononi. Kisha ndoa inaingia doa anapokosa kuhimili. Anapovumilia na saburi yake kulipa, anapata mwana kisha dunia inamchukua  mtoto wake wa pekee. Ni pigo linalohitaji moyo wa jiwe kustahimili.

UCHUNGU WA MWANA na Hadithi Nyingine ni antholojia iliyofumwa kwa miyaa  ya  lugha ashirafu  na nyuzi za misamiati ya kuhusudiwa. Imeyamulika  waa  maisha ya sasa   na kuyaweka peupe ya jana na kesho. Visa vyote vimeshiba fani aula na aali zitakazomfanya msomaji kutokinai kwa haraka.

Imejumuisha waandishi wenye ukwasi na ustadi kamili  wa lugha na wanaoelewa masuala mtambuko  na yanayoibuka katika maisha ya sasa. Inajivunia anwani zenye mvuto na maudhui yenye utajiri mkubwa wa lugha na mafunzo. Diwani hii inafunza, inaadibu, inaadili, inaonya na kutahadharisha jamii dhidi ya tamaa, ubinafsi na  mambo hasi yanayoikwaza jamii husika.

Wahariri wake wameivalia njuga na kuihakiki kwa makini ili kupakulia wasomaji uhondo wa fasihi isiyowekeka chini. Ustadh Kamau na Kaka Fred ni mfano aula wa wahariri mahiri wa fasihi. 

 

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “UCHUNGU WA MWANA na Hadithi Nyingine”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

No more offers for this product!

General Inquiries

There are no inquiries yet.